OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
BARAZA LA JIJI LA ZANZIBAR

BODI ZA USIMAMIZI
BODI YA ZABUNI BARAZA LA JIJI ZANZIBAR (2021)
Bodi ya Zabuni ya Baraza la Jiji la Zanzibar imeazishwa mwaka 2021 kwa mujibu wa sheria No. 11, 2016 na Kanuni ya mwaka 2021ya Ununuzi na Uondoshaji Mali za Umma Kwa mujibu wa Kanuni hiyo kifungu 27 (1) kila taasisi, kitengo, shirika na serikali za mitaa zinazofanya manunuzi huduma na kazi zinahaki ya kuazisha bodi ya zabuni. Kanuni katika kifungu cha 27(2) imeeleza Wajumbe katika bodi ya zabun isiwe chini y… na wasizidi wajumbe watano, kanunu 2021
Bodi ya Zabuni ya Baraza la Jiji ina wajume watano, ambao ni:
- Mwenyekiti – Afisa Mwandamizi kutoka Baraza la Jiji la Zanzibar
- Wajumbe watatu wanaotoka Baraza la Jiji la Zanzibar
- Mjumbe kutokawa Wizara ya Fedha na Mipango
MAJUKUMU YA BODI YA ZABUNI YA BARAZA LA JIJI LA ZANZIBAR
- Kuidhinisha zabuni na nyaraka za mikataba
- Kupokea na kufungua zabuni
- Kupitia mapendekezo kutoka kitengo cha ununuzi na kuchangua mshindi wa zabuni.
- Kuidhinisha kamati ya tathimini.
- Kuidhinisha kamati ya kufanya makubaliano.
- Kutathimini na kuhakiki mali za serikali zilizoorodheshwa na idara husika au bodi ya ukanguzi kwa ajili ya kuondoshwa.
- Kupokea malizilizoorodheshwa chini ya aya ya (g) kufanyiwa uthamini kwa mujibu wa kanuni zitakazotungwa chini ya sheria
- Kuidhinisha bei iliyowekwa kwa ajili ya mali zinazotaka kuondoshwa.
- Kuidhinisha taratibu za ununuzi na uondoshaji wa mali za umma
- Kuhakikisha kwamba sheria hii inatekelezwa
- Kuidhinisha taarifa ya tathimini ya zabuni kiufundi na fedha
- Kushirikiana moja kwa moja na mamlaka juu ya masuala ambayo yamo ndani ya mamlaka yake .
MAJUKUMU YA KAMATI YA UKAGUZI
Kamati ya Ukaguzi Baraza la Jiji la Zanzibar ina wajibu na majukumu yafuatayo kama ilivyoelezwa katika kanuni za Usimamizi wa Fedha za Umma, 2021 kanuni ya 149 (1), (2) kifungu kidogo a-n, ikiwemo
- Kuidhinisha mpango mkakati, mpango wa ukaguzi na mkataba wa ukaguzi kwa Kitengo cha Ukaguzi wa ndani wa Taasisi husika
- Kupitia taarifa za wakaguzi wa Ndani na taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
- Kufanya tathmini ya uwepo wa mifumo ya udhibiti wa ndani kwa taasisi husika
- Kujadili kwa pamoja na Afisa Masuuli matokeo na mapendekezo ya ukaguzi
- Kupitia na kufanya ufuatiliaji wa majibu ya uongozi na utekelezaji wa hoja na mapendekezo yaliyotolewa na Kitengo cha Ukaguzi wa ndani.
- Kutathmini mfumo wa udhibiti wa vihatarishi katika taasisi.
- Kupitia na kutoa mapendekezo kwa Sera ya Vihatarishi, mpango mkakati wa vihatarishi, mpango wa udhi