OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

BARAZA LA JIJI LA ZANZIBAR
Kamati ya kudumu
Nyumbani / Kamati ya kudumu
KAMATI YA KUDUMU YA BARAZA LA JIJI

Kamati itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati (atakaechaguliwa na Wajumbe wa Kamati husika na itakuwa na jukumu la msingi la kulishauri Baraza la Jiji katika masuala yote ya Kisheria. Kamati itakuwa na wajibu wa kupokea, kufuatilia na kufanyiakazi masuala ya kisheria ya Baraza la Jiji na itakuwa na wajibu wa kuwasilisha taarifa zake za utekelezaji za robo mwaka na za mwaka kwa Baraza la Jiji pamoja na kulishauri Baraza la Jiji ipasavyo kuhusu masuala yote ya kisheria na kuendesha Vikao vya Baraza.

Kamati itaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati (Mstahiki Meya wa Jiji) kutekeleza shughuli zote za Kamati zikiwemo za upokeaji na uidhinishaji wa taarifa za mapato na matumizi za Afisi ya Mkurugenzi wa Jiji za kila mwezi robo mwaka na mwaka. Kamati itakuwa na wajibu wa kuwasilisha taarifa za utekelezaji wake kwa Baraza la Jiji kwa kila robo mwaka na mwisho wa mwaka pamoja na kulishauri Baraza juu mambo yote yanayohusiana na mapato na matumizi ya Baraza.