OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
BARAZA LA JIJI LA ZANZIBAR

Idara
Nyumbani / Idara
IDARA ZA BARAZA LA JIJI LA ZANZIBAR
maelezo ya idara
Majukumu kwa ujumla ya idara
- Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za Serikali katika uendelezaji wa shughuli za ukuzaji Utalii, Viwanda na Uwekezaji katika Jiji la Zanzibar.
- Kutoa Elimu ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo walioko katika sekta binafsi katika Jiji la Zanzibar.
- Kupokea, kuchambuana kuunganisha taarifaza ki-sekta (za maendeleo ya viwanda, biashara na uwekezaji) katika ngazi ya Jiji na Manispaa na kushauri ipasavyo;
- Kufuatilia na kushauri usajiliwa Shughuli za Biashara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za Jiji (Business Activities Registration) kwa mujibu wa sheria na kuboresha mazingiraya kuwezesha biasharakwa madhumuni ya kurahisisha taratibu za kuanzisha biashara.
- Kubaini namna bora ya ushiriki wa Baraza na Manispaa za Jiji katika kuimarishashughuli za kitalii na uwekezaji katika Jiji.
- Kufanya tathmini na kutoa mapendekezo juu ya miradi inayosimamiwa na Manispaa za Jiji pamoja na Miradi ya Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali inayofanyika katika Jiji la Zanzibar.
Majukumu kwa ujumla ya idara
- Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za Serikali katika uendelezaji wa Mipango Miji, Uhifadhi wa Mazingira na Utoaji wa Huduma za Jamii katika Jiji la Zanzibar.
- Kushiriki katikakuandaa, kufanya mapitiona kuutekeleza MpangoMkuu wa Matumizi ya Ardhi (Master Plan) wa Jiji la Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali kuu kupitiaIdara yake ya Mipango Miji na Vijiji.
- Kuendeleza maeneo na mitaa ya zamani ya Jiji kwa kuifanyia Mipango yake ya uendelezaji (Urban Renewal plans/programme) kwa kushirikiana na Serikali kuu kupitia Idara yake ya Mipango Miji na Vijiji pamoja na Mabaraza ya Manispaa za Jiji.
- Kusimamia na kuratibu shughuli za maendelea ya ujenzi katika Jiji la Zanzibarkwa mashirikiano na taasisi nyengine za Serikali.
- Kuimarisha huduma za Jamii na mandhari ya Jiji la Zanzibar kwa kushirikiana na Idara nyengine za Baraza la Jiji na kutoa elimu na miongozo mbalimbali kwa watendaji wa Mabaraza ya Manispaa kuhusu uendelezaji wa Miji kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
- Kufuatilia na kutathmini athari za uchafuziwa mazingira katikamaakazi ya watu, viwanda,ujenzi, biashara, masoko,machinjio, gari za abiria na fukwe za Jiji.
- Kusimamia usafi wa mazingira na uimarishaji wa mandhari ya Jiji la Zanzibar.
- Kufanya tafiti na kubaini aina ya taka zinazozalishwa kutoka katika masoko, makaazi,maeneo ya biashara, na taasisi pamojana kubuni njia bora ya uhifadhi na matumizi ya taka.
- Kuyasimamia Mabarazaya Manispaa ili kuhakikisha Kamatiza Mazingira kuanzia ngazi ya mtaa, Shehia, Wadi na Manispaa zinatekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo suala la kutoa elimu kwa jamii
- Kuratibu na kusimamia kazi za Kamati ya Maendeleo ya Jiji Huduma za Jamii na Mazingira.
- Kutayarisha ripoti na kutoa mapendekezo ya utendaji wa kazi za Idara kwa vipindi vya robo mwaka na mwaka mzima na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi Mkuu wa Jiji kwa hatuazaidi.
- Kuanzisha ushirikiano na Majiji na Mashirika ya Kimataifa kwa lengo la kupata uzoefu juu ya shughulimbalimbali zinazohusiana na kazi za Idara na Baraza la Jiji kwa ujumla.
Majukumu ya ujumla ya idara
- Kuandaa na Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Rasilimali Watu na mfumo wa kupima utendajikazi kwa watumishi;
- Kuandaa IKAMA,kusimamia na kushughulikia masuala ya mishahara ya watumishi na stahiki za watendaji wa Afisi;
- Kuandaa na kusimamia mpango wa kuwajengea uwezo watendaji wa Afisi; Kufanya tathimini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa mipangoya mafunzo.
- Kusimamia mazingira ya kazi, usalama na mahitaji muhimu ya Afisi yakiwemo kutunza kumbukumbu za vifaa vya Afisi na kumbukumbu za watumishi.
- Kutoa huduma za kiutawala zikiwemo ulinzi, usambazaji wa barua na nyaraka mbali mbali za Afisi, usafiri, usafi, ukarabati na utunzaji wa majengo na mazingira ya Afisi.
- Kushughulikia masuala ya ajira, upandishwaji vyeo, kuthibitishwa kazini, uhamisho, mahusiano mahali pa kazi na kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi.
- Kuandaa, kuhuishana kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa Utoaji wa Huduma kwa wateja.
- Kutafsirina kusimamia sheria,kanuni namiongozo yakazi.
- Kutoa mwongozo na utaalamu wa uandaaji wa mipango, viashiria vya utekelezaji pamoja na taarifa za utekelezaji wa kazi za Afisi.
- Kuandaa mfumo na muundo wa ukusanyaji wa taarifa na ripoti za utekelezaji.
- Kuandaa mfumo wa ufuatiliaji na kutoa ushauriwa kitaalamu katika utekelezaji wake.
- Kukusanya taarifa mbali mbali, kufanya uchambuzi na kutambua masuala yanayopaswa kujumuishwa katika takwimu za Afisi.
- Kusimamia na kufanya Tathmini za Utekelezaji wa Miradi, Mipango, na Programu mbalimbali na kutambuamatokeo yake.
- Kusimamiana kufanyaufuatiliaji washughuli zaManispaa zaJiji.
- Kusimamiana kufanyaufuatiliaji washughuli zaManispaa zaJiji.
MAJUKUMU MAKUU
Majukumu makuu ya idara hii katika Baraza la Jiji la Zanzibar ni kama yafuatayo:
- Kuandaa na Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Rasilimali Watu na mfumo wa kupima utendaji kazi kwa watumishi.
- Kuandaa IKAMA, kusimamia na kushughulikia masuala ya mishahara ya watumishi na stahiki za watendaji wa Afisi.
- Kuandaa na Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Rasilimali Watu na mfumo wa kupima utendaji kazi kwa watumishi.