OFISI YA RAIS

TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ

BARAZA LA JIJI LA ZANZIBAR
Muundo wa kiutawala
Nyumbani / Muundo wa kiutawala
MUUNDO WA BARAZA LA JIJI UNAOPENDEKEZWA

Muundo wa Baraza la Jiji unaopendekezwa umezingatia matakwa ya Kisheria ya kutekeleza majukumu ya Baraza la Jiji, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa Shughuli za Manispaa za Jiji pamoja na kupunguza gharama za kuutekeleza muundo huo. Aidha, Sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa Nam. 07/2014 na marekebisho yake ya mwaka 2020 Kifungu Nam. 18(2)(d) na 18(2)(e) inafafanua zaidi. Baraza la Jiji linaundwa na Sehemu kuu mbili. Sehemu ya Kisiasa (Baraza la Madiwa la Jiji) itakayoongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji na Sehemu ya Kiutendaji (Afisi ya Mkurugenzi wa Jiji) itakayoogozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Jiji.