OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ
BARAZA LA JIJI LA ZANZIBAR

Dira na dhamira
Nyumbani / Dira na dhamira
DIRA, DHAMIRA NA MIKAKATI
Dira ya Baraza la Jiji la ZanzibarKuwa na Jiji la Zanzibar lenye mazingira bora na endelevu yanayowezesha utoaji wa huduma bora na za kuvutia kwa wananchi, wageni na wawekezaji ifikapo mwaka 2050.
Dhamira ya Baraza la Jiji la ZanzibarKuanzisha, kuendeleza na kusimamia miundombinu ya kisasa ya huduma za kiuchumi, kijamii na kimazingira, kwa kutumia vyema rasilimali zilizopo na teknolojia za kisasa kwa mfumo shirikishi
Mikakati mahsusi ya Baraza la Jiji la Zanzibar
Mpango Mkakati wa Baraza la Jiji umetaja mikakati mahsusi ya kiutekelezaji ili kuhakikisha kupatikana kwa mafanikio yaliyokusudiwa ndani wa wakati wa utekelezaji wa shughuli zilizopangwa. Mikakati hiyo ni pamoja na ifuatayo:
- Kuyasimamia Mabaraza ya Manispaa yaliyomo ndani ya Jiji la Zanzibar na kuhakikisha usafi na udhibiti wa taka unafanyika kwa kiwango cha kuridhisha ili kulifanya Jiji kuwa na mandhari ya kupendeza na kulinda afya za wakaazi wake.
- Kubuni vyanzo vya mapato na udhitibiti wa mapato kwa kutumia mifumo ya kielektroniki.
- Kuandaa mazingira bora ya yatakayowezesha kuimarisha maendeleo ya biashara, kukuza utalii, kuvutia uwekezaji na kuwakuza wajasiriamali.
- Kuimarisha uwezo wa taasisi na kukuza mahusiano na mashirikiano na jamii pamoja na taasisisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
- Kuhakikisha shughuli zote za Baraza la Jiji la Zanzibar zinafanyika kwa kuzingatia Utawala Bora na kuzingatia Sera, Sheria na Miongozo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.